Semina kwa vijana katoliki kigango cha Kinyanambo c
DEC
17
SEHEMU YA I
(Kijana wa parokia ya mjini uko wapi)?
“FANYA MAAMUZI”.
Tuna mshukuru Mungu kutulinda kwa kipindi chote cha mwaka huu unaomalizika sasa.
Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya Kiongozi wetu Baba mt. aliyetutangazia mwaka wa huruma ya
Mungu naamini kila mmoja wetu amefaidika kwa kipindi hiki pekee. MAISHA YA HURUMA NA
MSAMAHA NDIO MAISHA YA MKRISTU hasa Mkatoliki.
MADA ZETU
1. KIJANA KATIKA HALI YA KUJITAMBUA
2. KIJANA NA MAISHA YA SAKRAMENTI
3. KIJA NA MAHUSIANO.
4. VIDEO (kama miundo mbinu inaruhusu)
1. KIJANA KATIKA HALI YA KUJITAMBUA
Somo WAEFESO 5:1-18. (Kuishi katika Kristo) TAFAKARI FUPI …………………………………………
Maisha mapya ya kijana
Kuishi kama watu wa Mungu na maisha ya kumpendeza Mungu. (Waefeso.5:3)
Msikubali kudanganywa na mtu kwa maneno matupu (pia kwa fedha na mali!!) Waefeso 5:6
(ni kwa nini sisi vijana hasa wakatoliki mnakuwa rahisi sana
kudanganyika)?.....................abuja declaration 1989…..effects on africa and the world. SALA
ZA NGUVU NA SALA-maamuzi.
Sasa amka wewe uliye lala, na ufufuke kutoka wafu nae Kristo atakuangaza.
Kijana unaamshwa usingizini leo. Kipindi hiki cha Kanisa cha majilio je umejiandaaje? Umejipangaje?
MAANA YA MAJILIO KWA UFUPI
Majilio (pia: Adventi) ni kipindi cha liturujia ya madhehebu mbalimbali ya Ukristo (kama vile Kanisa
Katoliki, ya Waorthodoksi, Waanglikana na Walutheri) kinatangulia sherehe ya Noeli na kuanza
mwaka wa liturujia. Kinaweza kudumu kati ya siku 22 na 40.
Jina lake kwa Kilatini ni adventus maana yake ujio (wa Yesu Kristo), lakini jina la Kiswahili ni sahihi
zaidi kwa sababu linadokeza kuwa ujio wa Yesu ni kwa ajili yetu na kuwa alikuja zamani, anakuja kila
siku na atakuja kwa utukufu mwisho wa dunia.
KWA NINI KUWEPO NA MAJILIO ?
Sisi binadamu hatuwezi kuishi daima katika hali ileile bila ya matazamio. Hasa kijana anatarajia
mambo mapya tena mema. Hivyo tunajitahidi kuyapata. Asiyetazamia chochote amevunjika moyo,
hana hamu ya kuishi. Lakini matazamio ya kibinadamu yakimfikia mtu hayamridhishi moja kwa
moja. Kristo tu anatimiza hamu zote kwa kumkomboa kutoka unyonge.
Majilio yanatukumbusha kila mwaka matarajio ya kweli na hivyo yanaamsha hamu ya kuishi kwa
bidii ya kiroho.
MWAKA 2016 UMEFANYA NINI?
Huu ni mwezi wa 12/2016. Tangu January . tunamaliza mwaka sasa. wewe kama kijana mkatoliki
umeweza kufanya nini?
a. Kwa maendeleo yako ya kimaisha?. Je nimetimiza ya yangu ya msingi?( ya lazima? Hapa
kuna mambo MATATU tuwe makini.
I. Kuna mambo ya msingi YA LAZIMA. MF Elimu, ujuzi, kumjenga kujijenga
II. KUNA MAMBO MUHIMU( SI YA LAZIMA) mf.kuwa na simu, kusomea lugha nyingi,
kuwa na gari, kuoa na kuolewa,
III. KUNA MAMBO YA KIFAHARI (SI YA LAZIMA) mf. Kuwa na nyumba nzuri, vitu vya bei
ya juu; cm ya bei ya juu….na mambo kama hayo…
b. Kwa faida ya wale wanaokuzunguka? Mfano familia yako
c. Kwa bidii katika kukua kiroho? Je umeachia tu mwaka huu upite? (Pigamaesabu)
Umewekaje mahusiano yako kipindi chote cha mwaka huu wewe na Mungu wako?
Umeweza kufanya yale ya msingi anayotaka Mungu au umejifanyia ya kwako?
Ni vizuri sasa kjiweka tayari kwa mwaka ujao usijekuwa mwaka wa majuto na
masononeko.
Matarajio yako yamekamilika au ulikata tama?
Ni vema kujiuliza ndio mtu uweze kupiga hatua inayofuata.
Waefeso6:1ff “enyi watoto watiini wazazi wenu Kikristo maana hili ni jambo jema. Je
nimeyatenda hayo? Nimewaheshimu wenzangu?, nimewajali wenzangu?
Nimesababisha madhara kwa mwenzangu kiasi gani? Je nimeoomba msamaha?
d. Nijiwekee malengo mwa 2017.
Mshirikishe Mungu katika maisha yako. (Jermiah 33:3) “niite nami nitakujibu na
kukuambia mambo makubwa yaliofichika ambayo hujapata kuyajua”.
Munguhatakufanya udhauliwe tena (YOEL 2:19b)
3
Fr Haki semina ya vijana Dec.10/12/2016
Maswali kama yapo……………….
SEHEMU YA II
2. KIJANA NA SAKRAMENTI YA KITUBIO
Mara nyingi sakramen ya Kitubio ndio huwa inachangamoto nyingi sana na kwamba watu wengi
hawaipokei. (jiulize mara mwisho ulipo ipokea je ilkuwa kwa usahihi wake?
Sakramenti ni miferji ya neema kwa hiyo ni lazima ziwe na changamoto.
Tuangalie changamoto hizi kwa miwani ya kijana wa leo. Kijana anatatizo kubwa kuielewa na kuithamni
sakramenti hii ya upatanisho. Tutaje tu baadhi ya vikwazo;
Kijana wa leo hana imani kuwa Mungu kweli anaweza kumsamehe dhambi. Ni wasi wasi ambao
unajengwa na jinsi anavyorudiarudia kuanguka katika katika dhambi. Ila Kristu alitufundisha
kusamehe mara ngapi? Je wewe ulishawahi kumkosea Mungu mara mia nne na sabini? Usikate
tama “Tukikumbushe “Haya njooni tusemezane, asema Bwana, dhambi zenu zijaapokuwa
nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera zitakkuwa
kama sufu” (Isaya.1:18).
Kijana wa leo haoni umuhimu wa Sakramenti ya wongofu. Tatizo ni nini? Labda haoni tatizo. Je
unaweza kula chakula bila kunawa mikono?.....kadiri unavyojitahidi kimwili kuwa safi basi pia
tunahitaji kuwa safi KIROHO. AU wataka upate kipindupindu cha kiroho?
Kijana wa leo anaishi kwa HOFU. Nikienda kuungama Padri atanijua kuwa mimi ni mdhambi.
Tena ni kujidhalilisha watu wakiniona nikisubiri zamu yangu….kwanini tunaanza kuwa na hofu
baada ya kutenda dhambi? Hofu ya kweli ingetushtua na kuacha kutenda dhambi. Kujidhalilisha
ingekuwa ni pale tunapoanguka dhambini….iweje isiwe kujidhalilisha unaposubiri kuingia
kwenye danguro wamsubiri mwenzako na iwe unaposubiri kuungama?..kama upo hodari wa
kutenda dhambi , yakupasa kuwa shujaa wa kuungama.
Kijana wa leo analalamika sana. Kwa familia zetu neno msamaha ni nadra sana. Kosa likitokea
anatukanwa,kupigwa…kafundishwa kusamehe…tujilelee ktka mazingira ya kusamehe ndio
zawadi kubwa tunawezotoa.
Kijana wa leo anaogopa kuungama kwa hofu ya kuchemsha. Hakumbuki tena namna ya
kuungama.
Kijana wa lwo anazungukukwa na watu wa imani mbalimbali anasoma vitabu na magazeti
yenye mitazamo tofauti. Usimwige mwenzako….!!!
Kijana wa leo anayumbishwa na mtazamo wa jamii. Neno “dhambi” katika jamii halina tena
maana. Limepitwa na wakti. Kosa kuwa kosa siku hizi ni mpaka ukamatwe. Jiunge kwenye vyama
vya kitume usifikiri wao ni wadhambi zaidii….
Kijana wa leo anazungukwa na utamaduni wa uovu. Jamii imehalalisha mengi,kila kitu ni ruksa
kama kinakupendeza….mengine yamepewa majina ili kufisha uhalisia..mf. TENDO LA NDOA
lilipewa jina hilo ili kuonesha nani hasa anastahili ila kwa sasa lina majina mengi kama uroda n.k
kuonesha ni jinsi gani tunapenda vitamu tamu!! Uongo unaitwa….soga, wizi unaitwa kusogeza,
daya ya kulevya inaitwa unga, rushwa inaitwa toa kitu kidgo, hayo ndio maisha ya leo,kutoa
mismba kunaitwa kusafisha, kushusha ingini n.k kijana anazongwa na mambo mengi sana ni
lazima kuwa makini sana. Kijana unakwenda na fasheni, unakwenda na wakati wakati gani?
Heri uende na wa kati wa kufa na kufufuka kuliko wakati wa kufa na kuoza.
Baba nae anaitwa ‘dadi’ .Funguka kijana. (Mt. 9:2) “Jipe moyo mwanangu, umesamehewa
dhambi zako”
SEHEMU YA III
3. KIJANA NA MAHUSIANO.
Krismasi na sherehe zake huleta furaha sana kama umejiandaa vyema na wengi huishia katika kujuta
pia maana wanashereheka kupita kiasi.
Kijana ni lazima aweze kutofautisha mambo haya.
Urafiki na uchumba……majina yanayotumika
Uchumba- maisha ya uchumba
Uchumba sugu-kuishi gizani, kwenye matope
Kijana ni lazimza aweze kujichaguliwa mwenza wake bila msukumo wowote na baada ya
maandalizi mazuri. (msibake ndoa)
Ni lazima kuwa na mawazo chanya kwa mwenzako na kutamani mwenzako afanikiwe kama
wewe.
Kuchagua mchumba hapa kuna kazi kwel kweli. Ila basi mpe Mungu nafasi katika kumchagua
mwenza wako usijeingia matatani. MZIKI MARRY ME….
Maisha ya kujaribu ndo inamadhara gani?
-mimba za utotoni
-Kutoa mimba
-Kutumia madawa (visibiti mimba) ambayo madhara yake mwayajua mnaotumia ni
makubwa sana.
Maswali kama yapo.
SEHEMU YA IV -FILM USINIUE.
Maisha ya ndoa ni maisha matakatifu, ndoa iheshimiwe, isichezewe, ndoa ni
sakrmenti. Mungu ameiweka kwa malengo maalumu ya uumbaji na si
KUJIFRUHISHA.
MWISHO…..MUNGU AWABARIKI NYOTE NA MERRY XMASS.
Posted 12th December 2016 by NIC
0 Add a comment
Loading